• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Syria limedhibiti asilimia 70 ya sehemu za mashariki mwa mji wa Aleppo

    (GMT+08:00) 2016-12-07 18:23:41

    Jeshi la serikali la Syria linadhibiti asilimia 70 ya sehemu za mashariki mwa mji wa Aleppo baada ya kurudisha udhibiti wa wilaya tatu muhimu za mji huo zilizokuwa zikidhibitiwa na waasi kufuatia mapambano makali ya nusu mwezi.

    Habari zinasema, jeshi hilo limedhibiti wilaya ya Shaar katikati ya mji huo ambayo ni muhimu kimkakati, pia limewaua magaidi wengi na kudhibiti ghala la kuhifadhia vitu vyenye sumu kali.

    Wizara ya mambo ya nje ya Syria imesema, jeshi hilo litaendelea na mapambano mpaka wapiganaji hao watakapoondoka kwenye mji humo.

    Wakati huohuo, wizara ya mambo ya nje ya China imesema, China kupiga kura ya veto dhidi ya mswada wa azimio kuhusu Syria kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kunatokana na msimamo wake wa kudumu katika suala hilo, na kwamba China itaendelea kushiriki kwenye mchakato wa utatuzi wa kisiasa wa suala la Syria na kupenda kutoa jitihada kutuliza hali ya mvutano iliyopo nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako