• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la chini la bunge la Uingereza launga mkono nchi hiyo kuanzisha mazungumzo ya kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2016-12-08 18:24:06

    Baraza la chini la bunge la Uingereza limepiga kura na kuunga mkono mpango uliotolewa na waziri mkuu wa nchi hiyo Bi. Theresa May kuhusu serikali kuanza mazungumzo ya kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya kabla ya mwezi Machi mwaka ujao.

    Makubaliano kati ya serikali na baraza la chini kuhusu "ratiba ya kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya" kunamaanisha kuwa Uingereza imepiga hatua muhimu katika kujitoa rasmi kwenye Umoja huo.

    Hii ni mara ya kwanza kwa baraza la chini kutoa msimamo wazi wa kuunga mkono baada ya serikali kutangaza ratiba ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya mwezi Oktoba mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako