• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • "Bibi wa binadamu" alikuwa na uwezo mkubwa wa kupanda miti

  (GMT+08:00) 2016-12-09 09:13:08

   

  Mabaki ya mifupa ya binadamu wa kale ambaye amepewa jina la Lucy na kusifiwa kuwa "bibi wa binadamu" ni moja kati ya mabaki ya binadamu wa kale yaliyo kamili zaidi. Watafiti wa Marekani wamekagua mabaki hayo na kugundua kuwa ingawa Lucy aliweza kutembea kwa miguu yake ardhini, lakini alikuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kupanda miti, na aliishi juu ya miti kwa muda mrefu.

  Mwaka 1974, wanaakiolojia waligundua mabaki ya mifupa ya Lucy nchini Ethiopia. Utafiti unaonesha kwamba Lucy aliishi katika miaka milioni 3.2 iliyopita, alikuwa na urefu wa mita 1.1 na uzito wa kilo 29. Katika miaka mingi iliyopita, watafiti walikuwa na maoni tofauti kuhusu kama Lucy alikuwa anatembea kwa miguu siku zote au la.

  Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins na Chuo Kikuu cha Texas wamepima mifupa yake kwa teknolojia ya kisasa, na kuilinganisha na ile ya binadamu wa kisasa na ya sokwe. Sokwe anaishi juu ya miti kwa muda mrefu, na anatembea kwa kutumia mikono na miguu kwa pamoja.

  Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa ingawa Lucy alikuwa mfupi, lakini alikuwa na misuli yenye nguvu kwenye mikono na miguu yake. Mikono yake inafanana zaidi na sokwe badala ya binadamu. Aliweza kutembea kwa miguu tu, lakini hakutembea vizuri na kwa muda mrefu kama binadamu wa kisasa wanavyofanya.

  Watafiti wamekadiria kuwa binadamu wa kale waliishi juu ya miti kwa muda mrefu, hali hii huenda iliendelea kwa mamilioni ya miaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako