• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watafiti wavumbua betri inayozalisha umeme kwa almasi na takataka ya nyuklia

  (GMT+08:00) 2016-12-12 15:12:11

  Chuo Kikuu cha Bristol cha Uingereza kimeonesha betri inayozalisha umeme kwa almasi na takataka za nyuklia. Lakini teknolojia hii bado iko kwenye kipindi cha majaribio, na matatizo mbalimbali bado hayajatatuliwa.

  Watafiti wameweka rasilimali inayotoa mionzi ndani ya almasi iliyotengenezwa na binadamu ili kuzuia mionzi isivuje nje. Sasa wametumia rasilimali inayotoa mionzi ya Nickel-63 kutengeneza betri hii, lakini wanaendelea kufanya majaribio kwa kutumia rasilimali ya Carbon-14 ili kuongeza ufanisi wa kuzalisha umeme. Kwa nadharia watu wataweza kukusanya Carbon-14 kutoka kwenye takataka za nyuklia.

  Dr. Neil Fox amesema ni hatari kwa ngozi ya binadamu kuvuta mionzi inayotoka kwenye Carbon-14, lakini almasi ni kitu kigumu zaidi kinachoweza kuwalinda watu kutodhuriwa na mionzi.

  Tatizo la sasa ni kwamba ni vigumu kutengeneza betri hiyo, na gharama ya kuitengeneza ni kubwa. Lakini jambo zuri ni kwamba betri hii haileti uchafuzi mwingine na inaweza kufanya kazi kwa zaidi ya miaka elfu moja.

  Watafiti wanaona teknolojia ya kutengeneza betri hii ikipevuka, huenda ikatumiwa katika chombo cha kusukuma mapigo ya moyo, satilaiti na chombo cha safari ya anga ya juu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako