• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw Guterres aapishwa kuwa katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2016-12-13 10:13:42

    Bw. Antonio Guterres ameapishwa kuwa katibu mkuu wa awamu ya 9 wa Umoja wa Mataifa, na anatarajiwa kuanza kazi mwanzoni mwa mwaka kesho.

    Bw. Guterres ameapa kuwa atatekeleza wajibu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa utiifu, umakini na kwa kufuata maadili, na kuhudumia maslahi ya umoja huo. Amesisitiza kuwa Umoja wa Mataifa ni jiwe la msingi kwa utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi, na ni lazima uongeze nguvu katika kuzuia misukosuko. Amesema kazi zake kuu zitakuwa kuleta amani duniani, kusukuma mbele utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu na kuhimiza mageuzi ya Umoja wa Mataifa.

    Kwenye Baraza kuu la umoja wa mataifa Bw. Ban Ki-moon amejumuisha changamoto mbalimbali zinazoukabili Umoja wa Mataifa wakati akiwa madarakani, na kutoa shukrani zake kwa uungaji mkono wa nchi zote kwa kazi zake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako