• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Messi akutana na mtoto aliyevaa jezi ya karatasi Afghanistan

    (GMT+08:00) 2016-12-14 09:25:38

    Murtaza Ahmad mtoto mwenye umri wa miaka 6 kutoka nchini Afghanistan aliyepata umaarufu sana kwenye mitandao duniani mwezi Januari mwaka huu baada ya kupigwa picha akiwa amevalia mfuko wa nailoni aliotengeneza kama jezi ya Lionel Messi hatimaye amefanikiwa kukutana na Lione Messi.

    Kukutana kwa Messi na Murtaza kumetangazwa na Kamati ya Matayarisho ya Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2022 za Qatar ambao ndio waliandaa safari ya Mtoto huyo kwenda Doha.

    Timu ya Barcelona ilikuwa nchini Qatar kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Al Ahli ya Saudi Arabia na kufanikiwa kuitwanga kwa mabao 5-3.

    Katika mechi hiyo ya kirafiki, Luiz Suarez, Lionel Messi na Neymar kila mmoja alifunga bao moja kabla ya wote 3 kutolewa katika dakika ya 32.

    Kocha Luis Enrique aliwatoa wakali wake hao kwa kuwa wana mechi ngumu ya La Liga Jumapili dhidi ya Espanyol ambayo hujulikana kama Catalan Derby.

    Kwenye mchezo huo, mtoto Murtaza aliingia na Messi wakati timu hizo zilipokuwa zikiingia uwanjani kuanza mechi hiyo ya kirafiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako