• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasisitiza mwito wa kuondoa ajali za barabara barani Afrika

    (GMT+08:00) 2016-12-14 10:07:14

    Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya usalama barabarani Bw. Jean Todt amesema serikali za Afrika na wadau wanapaswa kufuatilia kwa makini tatizo la ajali za barabara, na kuzichukulia kama msukosuko wa afya ya umma unaoathiri maendeleo ya bara hilo.

    Bw Todt amezitaka nchi za Afrika kuimarisha utekelezaji wa sheria, kuboresha miundombinu na kuinua ufahamu wa umma ili kupunguza vifo vya watu kwenye ajali za barabarani.

    Akiongea mjini Nairobi kwenye warsha ya wiki ya usalama barabarani, Bw. Todt amesema tatizo la ajali za barabarani barani Afrika linapaswa kutatuliwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kukamilisha sheria husika, kujenga miundo mbinu yenye usalama zaidi na kutoa huduma bora baada ya kutokea kwa ajali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako