• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waasi wa Syria hawajaondoka Aleppo kama wanavyotakiwa kwenye makubaliano

    (GMT+08:00) 2016-12-15 10:03:19

    Habari kutoka Aleppo zinasema mapambano makali yameanza tena mjini humo, na makundi ya waasi hayajaondoka eneo hilo kama ilivyofikiwa kwenye makubaliano na jeshi la serikali ya Syria.

    Mashuhuda wamesema jana asubuhi kuwa pande zote zilisimamisha operesheni za kijeshi, lakini waasi hawajaondoka Aleppo kwa wakati, na mapambano yalianza tena baadaye. Tume ya waangalizi wa Russia nchini Syria imesema makundi ya waasi yameshambulia tena kituo cha jeshi la serikali ya Syria, lakini waasi nao wamelishutumu jeshi la serikali kwa kuanza mashambulizi ya anga kwanza dhidi ya maeneo wanayodhibiti.

    Zaidi ya hayo, shirika la habari la Syria SANA limesema kundi la waasi limeshambulia kwa mizinga eneo la Aleppo linalodhibitiwa na serikali ya Syria, na kusababisha vifo vya raia saba na wengine makumi kujeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako