• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya maendeleo ya Afrika yaidhinisha mkopo wa dola milioni 93 kwa ajili ya sekta ya kilimo Tanzania

    (GMT+08:00) 2016-12-16 09:08:53

    Benki ya maendeleo ya Afrika AfDB imeidhinisha mkopo wa dola za kimarekani milioni 93.51 kwa Tanzania ili kuunga mkono maendeleo ya sekta ya kilimo.

    Taarifa iliyotolewa na benki hiyo inasema, fedha hizo zitafikishwa kwenye Benki ya maendeleo ya kilimo ya Tanzania TADB, ambayo ni taasisi ya kifedha ya maendeleo yenye jukumu la kuendeleza sekta ya kilimo ya Tanzania, inayoajiri asilimia 67 ya watu nchini humo.

    Taarifa ya AfDB imesema, sekta ya kilimo inahitaji kuendelezwa zaidi, endapo Tanzania inataka kutimiza maendeleo endelevu.

    Taarifa pia imesema, ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa na ruwaza ya maendeleo ya Tanzania ya mwaka 2025, sekta ya kilimo ya nchi hiyo inatakiwa kukua kwa asilimia 10 kila mwaka. Lakini takwimu zinaonesha kuwa katika muongo uliopita, sekta hiyo ilikua kwa asilimia 4.4 tu kila mwaka na kuchangia asilimia 29.3 ya pato la taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako