• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Washiriki wa semina ya usalama wazitaka nchi za Afrika kuungana katika kupambana na ugaidi

    (GMT+08:00) 2016-12-18 19:12:16

    Washiriki wa semina ya ngazi ya juu ya 4 kuhusu amani na usalama barani Afrika wamezitaka nchi za Afika kuunganisha nguvu ili kupambana na ugaidi pamoja na biashara ya magendo katika bara hilo.

    Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa mwaka, ambaye pia ni Waziri wa mambo ya nje wa Chad Moussa Faki Mahamat ametoa ushauri kuwa hatua yoyote ya kijeshi katika mapambano dhidi ya ugaidi Afrika linatakiwa kuambatana na hatua kabambe za kisiasa,kijamii na kiuchumi.

    Naye waziri wa mambo ya nje wa Angola George Chikoti amewataka nchi za Afrika ambao si wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufikiria kuunganisha nguvu ili kuweza kuchangia katika maamuzi ikiwemo kujilinda uvamizi wa nje kwenye msuala ya ndani ya nchi za Afrika.

    Semina hiyo ya siku 3 ilianza jana jumamosi katika jimbo la Oran magharibi mwa Algeria, na inahudhuriwa na mawaziri wa mambo ya nje toka nchi mbalimbali za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako