• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatoa amri ya kuangalia uandikishwaji wa wakimbizi ili kuzuia kujiandikisha kwa mara mbili

    (GMT+08:00) 2016-12-19 20:44:11

    Serikali ya Kenya imetoa amri ya kuangalia upya orodha ya wakimbizi katika kambi ya Dadaab, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, ili kusaidia kuzuia wakimbizi kujiandikisha mara mbili, na pia kuwaondoa wadanganyifu.

    Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Joseph Nkaissery amesema, kuna matukio mengi ya wakimbizi kujiandikisha mara mbili, na kwamba kwa kuondoa watu hao kwenye kitabu cha usajili, kambi ya wakimbizi ya Dadaab itabaki na wakimbizi halali. Zoezi la kuwaondoa watu waliojiandikisha mara mbili kwenye kitabu hicho limeanza leo na linatarajiwa kumalizika tarehe 31 mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako