• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapongeza serikali ya Sao Tome na Principe kutambua sera ya kuwepo kwa China moja

    (GMT+08:00) 2016-12-21 20:00:31

    Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema nchi hiyo inashikilia sera ya kuwepo kwa China moja, na ina msimamo thabiti wa kupinga Taiwan kujitenga na China, ambao hakika utatambuliwa na kuungwa mkono zaidi na jamii ya kimataifa.

    Kauli hiyo imetokana na hatua iliyochukuliwa na serikali ya Sao Tome na Principe ya kusimamisha "uhusiano wa kibalozi" na Taiwan, na kusema serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ni serikali pekee halali ya China, na Taiwan ni sehemu isiyoweza kutengwa ya China.

    Mwaka 1971, kikao cha 26 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilipitisha azimio nambari 2758 likiamua sera ya kuwepo kwa China moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako