• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa kuweka mazingira ya kuanzisha tena mchakato wa kisiasa wa suala la Syria

    (GMT+08:00) 2016-12-22 17:49:48

    Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Wu Haitao amesema, jumuiya ya kimataifa inatakiwa kushirikiana zaidi na kuweka mazingira ya kuanzisha tena mchakato wa kisiasa wa suala la Syria mapema iwezekanavyo.

    Akishiriki kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wa kupigia kura muswada wa azimio la kuanzisha utaratibu huru wa kuwachukulia hatua za kisheria watu waliofanya uhalifu wa kivita nchini Syria, balozi Wu ametoa wito kwa pande zote za Syria kuzingatia mustakabali wa taifa na maslahi ya watu, kusimamisha vita na kutatua mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo.

    Bw. Wu pia amesema, China itaendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kusukuma mbele pande zote za Syria kurudia kwenye mazungumzo ya amani na kutafuta utatuzi unaokidhi mahitaji na kuongozwa na wasyria wenyewe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako