• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yarusha satelaiti ya kufuatilia utoaji wa hewa chafu duniani

    (GMT+08:00) 2016-12-22 17:59:39

    China imerusha satelaiti ya TanSat itakayofuatilia utoaji wa hewa chafu kutoka Kituo cha Kurushia Satelaiti cha Jiuquan kilichoko kaskazini magharibi mwa Jangwa la Gobi.

    Msanifu mkuu wa satelaiti hiyo Yin Zengshan amesema, satelaiti hiyo yenye uzito wa kilogramu 620, ilirushwa na kuingia kwenye mzunguko wa dunia karibu kilomita 700 juu ya dunia, na itafuatilia wingi, usambaaji, na mwenendo wa hewa chafu katika hewa.

    China ni nchi ya tatu kufuatilia utoaji wa hewa chafu kupitia satelaiti yake yenyewe. Nchi nyingine zilizotangulia kufanya hivyo ni Japan na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako