• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chelsea yapeta kileleni, Man U mambo safi, Wakati Arsenal

    (GMT+08:00) 2016-12-27 09:18:03

    Chelsea wamepaa Pointi 9 juu kwenye, Ligi Kuu England EPL baada kuichapa Bournemouth 3-0 kwa Bao za Pedro, Bao 2, na Penati ya Eden Hazrad huko Stamford Bridge na kujizatiti kileleni mwa ligi hiyo.

    Ushindi huu wa Chelsea ni wa 12 mfululizo kwenye EPL kwa Klabu hiyo na kujiwekea Rekodi yao wenyewe.

    Huko Old Trafford Manchester United wameitandika Sunderland 3-1 katika Mechi ya kwanza kwa David Moyes kwa mara ya kwanza tangu atimuliwe Umeneja na Man United Aprili 2014.

    Huu ni ushindi wa 4 mfululizo kwa Man U katika EPL na mabao yao yalipachikwa kimiani na Daley Blind, Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan aliyefunga goli zuri sana.

    Nako huko Emirates, Arsenal ilibidi wasubiri hadi Dakika ya 86 kwa Olivier Giroud kuwafungia bao pekee na la ushindi walipoitungua West Bromwich Albion 1-0.

    Mechi za EPL zitaendelea leo Jumanne kwa Mechi moja huko Anfield kwa Liverpool kuikaribisha Stoke City na kesho Jumatano Mechi moja kati ya Southampton na Tottenham.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako