• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama cha Ukombozi cha Palestina PLO chaunda tume ya ufuatiliaji kwa ajili ya kukomesha ukaliaji wa Israel mwakani

    (GMT+08:00) 2016-12-28 09:55:13

    Chama cha Ukombozi ya Palestina PLO kimetoa uamuzi wa kuunda tume ya ufuatiliaji ili kukomesha ukaliaji ardhi yake wa Israel katika mwaka kesho.

    Mwenyekiti wa chama cha PLO ambaye pia ni rais wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas amesema tume hiyo itachukua hatua halisi ili kumaliza ukaliaji wa ardhi yake unaofanywa na Israel.

    PLO kimesema tume hiyo itafuata azimio namba 2334 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, linalotoa mwito kwa Israel kuacha kujenga na kupanua makazi yake katika ardhi iliyotwaa mwaka 1967.

    Wiki iliyopita wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walipiga kura na kupitisha azimio la kuilaani Israel kukalia ardhi ya Palestina, na kutoa wito kwa Israel isimamishe vitendo hivyo. Nchi 14 zilipiga kura ya ndio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako