• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachukua hatua kupanua ufunguaji mlango na kutumia kwa ufanisi fedha za kigeni

    (GMT+08:00) 2016-12-30 18:17:25

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang hivi karibuni ameitisha mkutano wa kudumu wa baraza la mawaziri, mkutano ambao umekagua na kuthibitisha taarifa kuhusu kupanua ufunguaji wa mlango na kufanya juhudi za kutumia fedha za kigeni. Naibu mkurugenzi wa Kamati ya mageuzi ya maendeleo ya China Bw. Ning Jizhe ameeleza kuwa, China itaweka mazingira mazuri zaidi ya ushindani ulio na usawa kwa fedha za kigeni, kuhimiza duru mpya ya ufunguaji mlango kwa nje katika kiwango cha juu.

    Takwimu zimeonesha kuwa, katika miezi 11 ya mwanzo mwaka huu, kampuni zinazowekezwa na nchi za nje zimefikia 24,355, hili ni ongezeko la asilimia 3; matumizi ya fedha za kigeni yalifikia yuan bilioni 732, sawa na dola za kimarekani bilioni 113.8, hili ni ongezeko la asilimia 3.9. Inakadiriwa kuwa mwaka huu China itavutia fedha za kigeni zenye thamani ya RMB yuan bilioni 785, kiasi hicho kinaifanya China kushika nafasi ya kwanza kati ya nchi zinazoendelea katika miaka 25 iliyopita. Taarifa iliyotangazwa imesisitiza kuwa, China itarekebisha sera na sheria zinazohusika, ili kuzidi kupanua ufunguaji mlango. Naibu mkurugenzi wa Kamati ya mageuzi ya maendeleo ya China Bw. Ning Jizhe anasema:

    "Taarifa imetangaza hatua 20 kuhusu kuzidi kupanua ufunguaji mlango, kuzidi kuweka mazingira yaliyo na usawa ya ushindani, kuzidi kuimarisha kazi ya kuvutia fedha za kigeni pamoja na sera, na hatua zitakazochukuliwa baada ya kuidhinishwa kwa uwekezaji wa wafanyabiashara wa nchi za nje, kulegeza masharti ya kuidhinisha fedha za kigeni, na kuongeza nguvu ya kuvutia fedha za kigeni."

    Wafanyabiashara wa nchi za nje wanafuatilia sana mazingira ya ushindani wa usawa. Akizungumzia suala hilo Bw. Ning Jizhe amesisitiza umuhimu wa kufanya ukaguzi na uthibitishaji juu ya ushindani wa usawa wa sera za fedha za kigeni, akisema:

    "Hivi sasa baraza la serikali la China linaagiza idara mbalimbali kufanya ukaguzi na uthibitishaji juu ya ushindani wa usawa wakati zinapotunga sera kuhusu fedha za kigeni na kukusanya maoni hadharani. Wakati huo huo linazitaka idara na sehemu mbalimbali kutekeleza kwa makini sera na kanuni za serikali, ili kuhakikisha sera zinazohusika zinatekelezwa kwa hatua za kudumu na kwa uwazi."

    Kati ya mwezi Januari na Novemba mwaka huu, thamani ya matumizi ya fedha za kigeni ya China iliongezeka kwa asilimia 3.9 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, lakini kasi ya ongezeko haijafikia nusu ya ile ya mwaka jana. Bw. Ning Jizhe ameeleza kuwa, hali hiyo imeonesha kuwa China na nchi za nje, zikiwemo kampuni zinazowekezwa na nchi za nje, zote zinafanya marekebisho ya kimuundo. Lakini China bado ni moja ya nchi zinazovutia uwekezaji kwa wingi zaidi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako