• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kipindupindu chaua watu watatu magharibi mwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-01-01 17:06:23

    Watu watatu wamefariki baada ya kuugua ugonjwa wa kipindupindu magharibi mwa Tanzania wilayani Tanganyika katika mkoa wa Katavi.

    Mwenyekiti wa kamati ya maafa wilayani humo, Salehe Muhando amesema ugonjwa huo ulianza Desemba 9 mwaka jana katika kata ya Kapalamsenga, na hadi sasa wilaya hiyo imeripoti taarifa za maambukizi ya ugonjwa huo kwa watu 91.

    Mhando ameeleza sababu mojawapo ya mlipuko wa ugonjwa huo ni kutokana na uhaba wa vyoo kwa baadhi ya makazi na kuwalazimu kujisaidia pembezoni mwa ziwa Tanganyika.

    Hata hivyo, amesema kuwa uongozi wa Wilaya umeanza kampeni kuhakikisha wanazuia magonjwa ya kuhara ikiwemo kuwazuia watu kutumia maji wanayotoa ziwani kwa ajili ya kupikia, kuoga na kunywa na badala yake kutumia maji ya bomba.

    Kampeni hizo zitasimamiwa na viongozi wa vijiji na kupiga marufuku mikusanyiko ya watu ikiwemo sherehe za harusi, mazishi na za kibiashara na kuagiza wale watakaokiuka maagizo hayo, kupigwa faini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako