• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Guardiola akaribia kustaafu kufundisha soka

    (GMT+08:00) 2017-01-04 09:09:47

    Kocha wa Man City Pep Guardiola amesema kuwa klabu hiyo inawezakuwa klabu yake ya mwisho kuifundisha baada ya kukasirishwa na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo wa jana dhidi ya Bournemouth.

    City, ilipata ushindi wa mabao 2-1, kwenye mchezo huo, uliochezwa uwanja wa nyumbani wa Man City wa Etihad, na kushuhudiwa na kiungo wake mkabaji Fernandinho akipewa kadi nyekundu.

    Guardiola, aliyesaini Man City kwa misimu ya miaka 3 na hadi sasa akiwa ndiyo kwanza ana miezi 6 na klabu hiyo, amesema asingependa kufundisha mpira hadi umri wa miaka 65, hivyo klabu hiyo ya Man City ni ya mwisho kwake kufundisha

    Muispania huyo amewahi kuifundisha klabu ya Barcelona kwa mafanikio makubwa kisha Bayern Munich kabla ya kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini Man city.

    Guardiola ameshinda vikombe 14 katika miaka minne akiwa na Barcelona, ikiwa ni pamoja na vikombe vitatu vya La Liga na viwili vya ligi ya mabingwa Ulaya.

    Alipumzika mwaka mzima kabla ya kujiunga na Bayern Munich na kuwaongoza kupata vikombe vitatu vya ligi kuu licha ya kukosa ligi ya mabingwa Ulaya

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako