• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe maalumu wa UN atoa wito wa amani kati ya Sudan na Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-01-05 10:51:26

    Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya Sudan na Sudan Kusini Bw Nicholas Haysom jana amesisitiza umuhimu wa kutimiza amani kwa pande zote kati ya nchi hizo mbili.

    Haysom amesema hayo baada ya kukutana na rais Omar al-Bashir wa Sudan mjini Khartoum. Amesema jumuiya ya kimataifa inafanya juhudi kurejesha uhusiano kati ya Khartoum na Juba, na kuitafutia Sudan Kusini fursa za maendeleo na utulivu.

    Haysom ameongeza kuwa nchi hizo mbili zinatakiwa kutimiza amani kwa pande zote kwa njia ya mazungumzo. Amesema, Sudan ikiwa ni nchi muhimu mwanachama wa Shirika la Maendeleo la Serikali za Nchi za Afrika Mashariki IGAD, inaweza kufanya kazi kubwa katika kuhimiza amani nchini Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako