• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanasayansi watoa wito kwa viwanda kupunguza utoaji wa takataka na hewa zenye sumu

  (GMT+08:00) 2017-01-05 16:31:45

  Kikundi cha utafiti kinachoongozwa na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Sheffield kimetoa ripoti kwenye gazeti la Scientific Reports la Uingereza kikitoa wito kuvitaka viwanda duniani kutumia malighafi endelevu zenye sumu chache zaidi ili kupunguza utoaji wa uchafuzi na kukabiliana na mabadiliko ya hewa.

  Watafiti wa kikundi hiki wamechambua athari ya utoaji wa takataka na hewa zenye sumu kwa mujibu wa data zilizotolewa na Marekani, na kugundua kuwa mambo mengi yanaathiri utoaji wa sumu hizi, yakiwemo kudidimia au kufufuka kwa uchumi, kuongezeka kwa idadi ya watu, mabadiliko ya matumizi, na muundo wa uzalishaji.

  Watafiti wamefahamisha kwamba kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2006, utoaji wa takataka na hewa zenye sumu ulipungua kwa asilimia 42 nchini Marekani. Hali hii inatokana na kuboreka kwa teknolojia za uchimbaji madini na mawe na usimamizi wa takataka.

  Watafiti wamesema utoaji wa hewa ya Carbon Dioxide umetiliwa maanani katika muda mrefu uliopita, lakini watu hawajafanya uchunguzi wa kutosha kuhusu utoaji wa takataka na hewa zenye sumu ambao pia una athari kubwa kwa mazingira. Utafiti wao utavihimiza viwanda kudhibiti utoaji wa uchafuzi huo, hasa vile vya uchimbaji madini na mawe vinavyotoa uchafuzi mwingi zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako