• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Serikali ya Tanzania yapanga kukopa Sh trilioni 2.1

    (GMT+08:00) 2017-01-05 18:01:20

    Serikali ya Tanzania iko kwenye mazungumzo na taasisi za kifedha ambazo zinakopesha ili iweze kuikopesha kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17.

    Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amesema hali hiyo inatokana na kuwepo kwa masharti magumu yanayowekwa na taasisi za kifedha za nje pamoja na nchi wahisani ambazo zimekuwa zinaikopesha serikali katika kutekeleza bajeti yake yake katika miezi mitano ya kuanza kutumika kwa bajeti ya mwaka huu wa fedha.

    Pia Serikali imesema kwamba ina matumaini kwamba hivi karibuni itakamilisha mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa lengo la kupata mkopo wenye masharti nafuu.

    Alisema Serikali ilitarajia kukopa mikopo ya kibiashara ya Sh trilioni 2.1 kutoka kwa taasisi mbalimbali za kifedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali, lakini kutokana na masharti magumu ikiwemo riba kubwa haikuweza kufanya hivyo.

    Dk Mpango aliongeza kuwa kwa sasa Serikali inaendelea na mazungumzo na Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Kuwait, Abu Dhabi na Jumuiya ya nchi zinazouza mafuta kwa wingi (Opec).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako