• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shambulizi la lori lasababisha vifo vya watu wanne mjini Jerusalem

    (GMT+08:00) 2017-01-09 09:34:08

    Waziri Mkuu wa Israel Bw Benjamin Netanyahu amesema mhusika wa shambulizi la lori kuparamia watu lililotokea mjini Jerusalem, na kusababisha vifo vya watu wanne na kujeruhi wengine zaidi ya kumi, ni mfuasi wa kundi la IS.

    Habari zinasema lori hilo liliwaparamia askari waliokuwa wanashuka kwenye basi, Mpaka sasa askari wanne wamefariki wakiwemo wanawake watatu na mwanaume mmoja, na wengine kadhaa wamejeruhiwa vibaya.

    Vyombo vya habari vya Palestina vimesema aliyefanya shambulizi hilo ni mkazi wa Jerusalem mashariki, ambaye alipigwa risasi na wanajeshi baada ya tukio. Na msemaji wa polisi wa Israel Bibi Luba Samri amelitaja shambulizi hilo kuwa la kigaidi, na kusema uchunguzi zaidi kuhusu shambulizi hilo unaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako