• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa zamani wa Iran afariki dunia

    (GMT+08:00) 2017-01-09 19:19:57

    Rais wa zamani wa Iran Akbar Hashemi Rafsanjani amefariki dunia jana kutokana na ugonjwa wa moyo.

    Katika ujumbe wake alioutoa jana, kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ameeleza huzuni yake kutokana na kifo hicho cha ghafla cha rafiki yake, mshirika wake, na mwenza wake wakati wa mapinduzi ya kiislamu ya mwaka 1979. Amesema kifo cha Rafsanjani ni pigo kubwa kwa kuwa alikuwa anategemewa sana katika kuunga mkono uongozi nchini Iran.

    Naye msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo amesema, China inatoa salamu za rambirambi kwa kifo cha rais wa zamani wa Iran, Akber Hashemi Rafsanjani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako