• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China ataka kuifanya reli ya TAZARA iwe njia ya ushirikiano na ustawi

    (GMT+08:00) 2017-01-09 20:38:44

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye yuko ziarani nchini Zambia jana amesema reli ya TAZARA ni "njia ya urafiki" na "njia ya uhuru" ya Afrika, na China inapenda kushirikiana na Zambia na Tanzania kuifanya reli hiyo iwe njia ya ushirikiano na ya ustawi.

    Bw. Wang Yi amesema, uendeshaji wa reli ya TAZARA pia unakumbwa na matatizo mengi, na kufanya ukarabati na kutia uhai kwa reli ya hiyo mapema kunaendana na maslahi ya pamoja ya watu wa China na Afrika. Viongozi wa China, Zambia na Tanzania wamefikia makubaliano kwamba, China itatoa mchango mpya katika maendeleo ya siku za baadaye ya reli ya TAZARA.

    Aidha, Bw. Wang Yi amesema, kwa sasa ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika una mabadiliko matatu mapya, kwanza ni mageuzi kutoka ushirikiano unaoongozwa na serikali na kuwa ule unaoongozwa na soko, pili ni kuboresha zaidi kutoka kwenye biashara ya bidhaa za kawaida na kuwa biashara ya kuongeza uwezo na utengenezaji, na ya tatu ni kubadilika kutoka miradi ya kawaida ya mikataba na kuwa ya uwekezaji zaidi, ujenzi, na ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako