• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Jamhuri ya Kongo akutana na waziri wa mambo ya nje wa China

    (GMT+08:00) 2017-01-11 10:16:21

    Rais Denis Sassou Nguesso wa Jamhuri ya Kongo jana huko Brazzaville alikutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye yuko ziarani nchini humo.

    Rais Nguesso ameishukuru China kwa uungaji mkono wake kwa maendeleo ya uchumi wa Jamhuri ya Kongo na kusema nchi yake inapenda kuendelea kuimarisha ushirikiano na China, itatekeleza kithabiti ahadi ilizotoa kwa China na kuunga mkono kithabiti msimamo wa China kwenye masuala yanayohusiana na maslahi ya China yakiwemo masuala ya Taiwan na Bahari ya kusini ya China.

    Bw Wang Yi amesema China na Jamhuri ya Kongo ni marafiki wa dhati, na China ina imani na mustakbali wa maendeleo ya Jamhuri ya Kongo na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, haswa ushirikiano wa uzalishaji viwandani.

    Siku hiyo Bw. Wang Yi pia amekutana na mwenzake wa Jamhuri ya Kongo Bw. Jean Claude Ngakosso, na kubadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya nchi zao na masuala ya kikanda na kimataifa wanayofuatilia kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako