• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kwa nini paka wanaonekana wavivu?

  (GMT+08:00) 2017-01-11 12:36:43

  Paka wanapenda kupumzika siku nzima, hasa wale wenye umri mkubwa. Je, paka hao ni wavivu?

  Paka ni wanyama muhimu wanaofugwa na binadamu. Idadi ya paka nchini Japan inakaribia milioni 10, na idadi hiyo imezidi milioni 70 nchini Marekani. Paka wanapevuka katika umri wa mwaka mmoja, na kwa kawaida umri wao hauzidi miaka 25. Paka mwenye umri wa miaka 11 ni karibu sana na binadamu mwenye umri wa miaka 60.

  Watafiti wa Japan wamekagua viungo vya mabega, viwiko na magoti vya paka 75 wenye umri kati ya mwaka mmoja hadi miaka 21. Wamegundua kuwa asilimia 30 ya paka wenye umri kati ya mwaka mmoja hadi miaka minne, asilimia 56.5 ya wale wenye umri kati ya miaka mitano hadi kumi, na zaidi ya asilimia 90 ya wale wenye umri zaidi ya miaka 11 wana ugonjwa wa viungo. Matokeo hayo yanaonesha kuwa ni rahisi zaidi kwa paka wazee kupata ugonjwa huo. Maumivu ya viungo huenda yamesababisha paka wazee kutopenda kutembea.

  Watafiti pia wamegundua kuwa sababu ya paka kupata ugonjwa wa viungo ni tofauti na ile ya binadamu, hivyo sasa bado hakuna dawa nzuri ya kutibu ugonjwa huo wa paka, isipokuwa dawa ya kupunguza maumivu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako