• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Nigeria zatakiwa kuimarisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati

    (GMT+08:00) 2017-01-12 10:53:36

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw Wang Yi amesema China na Nigeria zinatakiwa kupanua ushirikiano wa kiutendaji na kuimarisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati.

    Bw. Wang amesema hayo jana alipokutana na mwenzake wa Nigeria Bw. Geoffrey Onyeama mjini Abuja, na kusema ushirikiano kati ya pande mbili unaweza kuimarishwa zaidi, ili kuziletea China na Nigeria maendeleo na ustawi zaidi.

    Bw. Wang anafanya ziara nchini Nigeria ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano muhimu yaliyosainiwa na marais wa nchi hizo mbili, na kusaidia utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa katika Baraza la ushirikiano wa China na Afrika.

    Kwa upande wake, waziri wa mambo ya nje Bw Geoffrey Onyeama amesisitiza kwamba Nigeria itaendelea kushikilia sera ya China Moja na kudumisha urafiki na ushirikiano na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako