• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema malalamiko ya aluminum ya Marekani yanakosa msingi wa ukweli

    (GMT+08:00) 2017-01-14 20:15:41

    China imejibu malalamiko ya biashara ya Marekani dhidi ya sekta ya aluminum ya nchi hiyo ikisema shutuma hizo hazina msingi wowote.

    Marekani imewasilisha malalamiko ya biashara kwenye Shirika la Biashara Duniani WTO dhidi ya China ikidaiwa kuuza aluminum kwa bei ya chini kwenye soko la kimataifa.

    Wizara ya Biashara ya China imesema kwenye taarifa yake iliyotolewa katika tovuti kuwa China imesikitishwa na uamuzi huo wa Marekani lakini itashughulikia suala hilo kwa mujibu wa kanuni za WTO. Taarifa hiyo pia imesema soko la aluminum la China lina ushindani mkubwa na pia ni sekta ya kibiashara, na mikopo husika na ununuzi wa malighafi umeingizwa sokoni kikamilifu.

    Taarifa imeongeza kuwa uzalishaji wa kupita kiasi unaozikabili sekta fulani ni suala la kimataifa, ambalo chanzo chake ni ukuaji taratibu wa uchumi wa dunia na mahitaji madogo, hivyo hiyo ni changamoto ya pamoja inayopaswa kutatuliwa kupitia juhudi za pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako