• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Mataifa ya Afrika laanza kutimua vumbi nchini Gabon

    (GMT+08:00) 2017-01-15 17:01:33

    Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ilianza kutimua vumbi jana huko Gabon ambapo kwenye mechi ya ufunguzi wenyeji walishindwa kuwakaribisha vizuri wageni wao Guinea Bissau na kujikuta wakiambulia sare ya goli 1-1.

    Michuano hiyo iliyofunguliwa rasmi na rais wa Gabon Ali Bongo mjini Libreville, imeshuhudia timu ya Gabon ikitoa upinzani mkali katika kipindi cha kwanza hata hivyo Guinea Bissau ilijaribu kupapatua vikali. Goli la kwanza liliingizwa kimiani dakika ya 52 na nahodha wa Gabon Pierre Emrick Emilano. Kwa upande wa Guinea Bissau waliendeleza mashambulizi dhidi ya Gabon na hatimaye Juary Marinho kuchana wavu katika dakika ya 89 na kupelekea matokeo kuwa sare ya 1-1. Baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa mashabiki wa Gabon waliizomea timu yao kutokana na kutoridhishwa na matokeo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako