• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais mteule wa Gambia atarajiwa kuapishwa wiki hii

    (GMT+08:00) 2017-01-17 18:22:44

    Rais mteule wa Gambia Adama Barrow amesema ataapishwa alhamis wiki hii mjini Banjul kama ilivyopangwa, na kuanza kutekeleza majukumu yake ikiwemo kuunda serikali mpya.

    Bw. Barrow ameyasema hayo kwenye taarifa yake aliyoitoa jana kupitia msemaji wake. Pia amemlaani rais wa sasa wa nchi hiyo Yahya Jammeh kwa kuwakamata wanajeshi, askari na raia, akitaka waachiwe uhuru.

    Tume ya uchaguzi ya Gambia imemtangaza Bw. Barrow kuwa rais baada ya kushindi uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 2, Desemba mwaka jana kwa kupata asilimia 45.54 ya kura zilizopigwa. Lakini, Jammeh amekataa matokeo hayo na kudai uchaguzi huo ufanyike upya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako