• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xinjiang kutoa elimu bure ya shule za chekechea zinazofundisha kwa lugha mbili

    (GMT+08:00) 2017-01-17 19:37:30

    Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur unapanga kujenga shule 4,387 za chekechea zinazofundisha kwa lugha mbili katika maeneo ya vijijini mkoani humo ili kufanya elimu ya chekechea ya lugha mbili iwafikie watoto wengine laki 5.6.

    Kwa mujibu wa idara ya elimu ya mkoa huo, kati ya shule hizo zitakazojengwa au kupanuliwa, 3,223 zitakuwa katika eneo la kusini mwa mkoa huo, na kwamba serikali pia itatenga fedha zaidi kwa ajili ya kuajiri na kuwawezesha walimu wanaoweza kufundisha kwa lugha mbili kwenye shule hizo.

    Mkoani Xinjiang, elimu ya chekechea hadi sekondari ya juu inatolewa bure.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako