• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele kuhusu "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kufanyika mwezi Mei nchini China

    (GMT+08:00) 2017-01-17 20:59:14

    Rais Xi Jinping wa China amesema mkutano wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa kuhusu "Ukanda Mmoja na Njia Moja" utafanyika mwezi Mei mwaka huu mjini Beijing, China.

    Rais Xi amesema hayo alipohutubia mkutano wa mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani unaofanyika mjini Davos, Uswisi. Amesema mkutano huo utajadili mipango ya ushirikiano, kujenga fursa za ushirikiano na kunufaika kwa pamoja na matunda ya ushirikiano. Pia unalenga kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayokabili uchumi wa dunia na wa kikanda, na kutoa nguvu mpya kwa maendeleo ya pamoja na pia kufanya pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" liwanufaishe watu wa nchi mbalimbali.

    Rais Xi ameongeza kuwa nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 100 zimeeleza kuliunga mkono pendekezo hilo lililoanzishwa miaka mitatu iliyopita, ambapo nchi na mashirika zaidi ya 40 zimesaini makubaliano ya ushirikiano na China. Uwekezaji wa makampuni ya China kwa nchi zilizo kwenye Ukanda na Njia hiyo umefikia zaidi ya Dola za kimarekani bilioni 50, mfululizo wa miradi inayotekelezwa na kuzaa matunda, kuchangia maendeleo ya uchumi wa nchi mbalimbali na pia kutoa nafasi nyingi za ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako