• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mwenyekiti wa Baraza la uchumi duniani

    (GMT+08:00) 2017-01-18 09:37:29

    Rais Xi Jinping wa China jana huko Davos alikutana na mwenyekiti wa Baraza la uchumi duniani WEF Bw. Klaus Schwab.

    Rais Xi amesema mkutano wa mwaka huu wa Baraza la uchumi duniani unafuatilia kwa karibu hali ya kimataifa, na kuonesha njia za dunia kujikwamua kiuchumi. Amesisitiza kuwa washiriki wa mkutano huo wanapaswa kutoa ishara nzuri ili kuongeza imani ya watu kwa mchakato wa utandawazi duniani.

    Bw. Schwab amesema China imetoa uungaji mkono mkubwa kwa Baraza la uchumi duniani, na baraza hilo linapenda kuimarisha ushirikiano na China na kwenye utatuzi wa masuala yanayoikabili dunia nzima.

    Rais Xi pia alikutana na makamu wa rais wa Marekani Bw. Joseph Biden. Kwenye mazungumzo yao, rais Xi amesisitiza kuwa maslahi ya kimsingi ya China na Marekani na ya dunia nzima yanahitaji juhudi za pamoja za nchi hizo mbili, ili kujenga uhusiano tulivu wa ushirikiano wa muda mrefu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako