• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Roboti zinazofanana kabisa na binadamu zitatengenezwa lini?

  (GMT+08:00) 2017-01-20 09:53:31

  Katika tamthilia ya sayansi ya kubuniwa ya Marekani "Westworld", roboti zilizotengenezwa kwa teknolojia ya uchapishaji wa 3D zinaweza kuongea, kucheka, kulia na kuwa na hisia mbalimbali zinazofanana na binadamu. Je, roboti hizi zitaweza kutengenezwa katika siku zijazo?

  Roboti zinazofanana na binadamu zinahitaji kuwa na sura inayofanana na binadamu kwanza. Lakini kwanza pia tunahitaji kutilia maanani nadharia ya "Uncanny Valley". Nadharia hii iliyotolewa na mtaalamu wa roboti wa Japan Bw. Masahiro Mori inasema roboti ikifanana zaidi na binadamu, watu wanaipenda zaidi, lakini mfanano huo ukifikia kiwango fulani, hisia nzuri hushuka ghafla na kubadilika kuwa hofu, lakini mfanano huo ukiendelea kuongezeka, watu wataipenda tena.

  Kabla ya hapo, roboti ya Sophia iliyotengenezwa na kampuni ya Hansen ya Marekani ambayo inaweza kuonesha hisia 62 usoni iliwatisha watu wengi. Mfanano kati ya roboti hii na binadamu ndio uliopo kwenye kiwango kinachoelezwa na nadharia ya "Uncanny Valley".

  Teknolojia inayopata maendeleo ya kasi katika miaka ya karibuni inawawezesha watu kutengeneza roboti zinazofanana zaidi na binadamu, lakini kutengeneza roboti zinazofanana kabisa na bindamu bado kunahitaji ushirikiano kati ya wataalamu wa kompyuta, saikolojia, hisia na neva na wahandisi. Mtaalamu wa roboti wa Chuo Kikuu cha Arizona Bw. Heni Ben Amor alisema kutengeneza roboti zenye hisia bado kunahitaji muda mrefu. Lakini mtafiti wa akili bandia wa Marekani David Levy ana matumaini makubwa kuhusu mustakabali wa roboti, alisema ifikapo mwaka 2050, binadamu huenda wakaweza kuoana na roboti, ambazo zitakuwa na sifa zote nzuri zikiwemo uvumilivu, moyo mwema na utiifu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako