• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 100 wa kundi la Al Qaida wauawa katika mashambulizi ya anga yaliyoongozwa na Marekani kaskazini mwa Syria

    (GMT+08:00) 2017-01-20 19:22:12

    Kituo cha televisheni cha al-Mayadeen cha Kiarabu kimesema, wapiganaji 100 wa kundi la Nusra Front lenye uhusiano na kundi la Al Qaida wameuawa katika mashambulizi ya anga yaliyoongozwa na jeshi la Marekani katika maeneo yao mkoani Aleppo, kaskazini mwa Syria.

    Habari zinasema, kundi la Nusra Front lilikuwa linakusanya nguvu kufanya mashambulizi nchini Syria baada ya mazungumzo ya amani ya Syria yanayotarajiwa kufanyika mjini Astana, ambapo kundi hilo litakuwa moja ya ajenda zitakazojadiliwa.

    Wakati huohuo, kundi la IS limeharibu ukumbi wa kale wa maonyesho wa Roma na eneo la Tetrapylon lililoko mjini Palmya, katikati ya Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako