• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Jammeh wa Gambia apewa nafasi ya mwisho kuondoka madarakani kwa amani kabla jeshi halijaingilia kati

    (GMT+08:00) 2017-01-20 20:26:38

    Majeshi kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) yamesitisha safari ya kuingia Gambia jana usiku, ili kumpa rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh nafasi ya mwisho kuondoka madarakani kwa amani.

    Mwenyekiti wa Tume ya ECOWAS Marcel Alain Da Souza amesema, amri ilitolewa kwa askari hao kusitisha safari yao, kwa kuwa Jumuiya hiyo inapendelea zaidi majadiliano na diplomasia.

    Jeshi la Senegal, likiungwa mkono na askari kutoka nchi wanachama wa ECOWAS, liliingia Gambia jana mchana katika operesheni ya kijeshi inayolenga kumlazimisha rais Jammeh kukabidhi madaraka kwa Adama Barrow ambaye aliapishwa jana mjini Dakar, kuwa rais mpya wa Gambia.

    Wakati huohuo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. António Guterres jana alizungumza kwa njia ya simu na rais mpya wa Gambia Adama Barrow, ambapo pamoja na mambo mengine, alimpongeza kwa kuapishwa kuwa rais mpya wa Gambia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako