• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wana uwezo mkubwa zaidi wa kutambua nyuso kufuatia kuongezeka kwa umri

    (GMT+08:00) 2017-01-23 14:36:10

    Uhusiano wa kijamii ni muhimu sana kwa binadamu, na kutambua nyuso mbalimbali ni uwezo wa lazima wa kuwasiliana na wengine. Kama huwezi kukumbuka nyuso za watu, utakabiliwa na matatizo mengi. Inaonekana kwamba binadamu wana uwezo mkubwa zaidi wa kutambua nyuso za watu kuliko kutambua vitu vingine. Uwezo huo ni mkubwa sana hata mara kwa mara tunaona vitu vinavyofanana na uso kwenye vitu mbalimbali.

    Awali, wanasayansi waligundua kuwa idadi ya seli za ubongo zenye rangi ya kijivu inaongezeka hatua kwa hatua baada ya kuzaliwa, idadi hiyo inafikia kilele katika umri wa miaka 12, baadaye inapungua hatua kwa hatua. Inaonekana kwamba kupungua kwa seli hizi si jambo zuri, lakini hali halisi ni tofauti. Wakati seli hizi zinapopungua, neva zisizotumiwa zitaachwa, na ubongo wa binadamu utakomaa zaidi.

    Kwenye ubongo wetu kuna eneo linalofanya kazi ya kutambua nyuso za binadamu, ambalo linaitwa fusiform gyrus. Bibi Kalanit Grill-Spector na wenzake kutoka Chuo Kikuu cha Stanford cha Marekani wamegundua kuwa, tofauti na seli za kijivu, ukubwa wa eneo la fusiform gyrus unaongezeka kadri umri unavyoongezeka, eneo hili kwa watu wazima ni kubwa kuliko watoto kwa asilimia 12.6. Uwezo kuhusu uhusiano wa kijamii ni uwezo unaopatikana na binadamu katika umri mkubwa zaidi, hivyo mabadiliko ya eneo husika kwenye ubongo yanaendelea kwa muda mrefu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako