• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sera mpya za biashara za Rais Trump zinaweza kuathiri uchumi wa nchi nyingine

    (GMT+08:00) 2017-01-25 18:27:36

    Wasiwasi umeanza kuonekana kuwa kubadilika kwa ghafla kwa sera za biashara za Marekani chini ya serikali ya Rais Donald Trump kunaweza kuathiri uchumi wa baadhi ya nchi.

    Jumatatu Rais Donald Trump alitangaza Marekani kujitoa kwenye makubaliano ya biashara ya nchi za Pacific TPP, na kusema anapanga kujadili upya makubaliano ya biashara ya nchi za Amerika kaskazini NAFTA na Canada na Mexico, ili kuinufaisha zaidi Marekani.

    Chama cha wapigania uhuru cha Afrika Kusini EFF kimesema urais wa Donald Trump una madhara kwa uchumi wa Afrika Kusini, na kusema ushindi wake ni tishio kwa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa kijinsia, chuki dhidi ya wageni na maendeleo ya dunia.

    Amesema sera ya kujilinda ya Marekani itaathiri uuzaji wa matunda ya Afrika kusini nchini Marekani, na kuathiri ongezeko la uchumi na ajira nchini Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako