• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwanahistoria maarufu asema teknolojia ya kuweka vyombo vya elektroniki kwenye mwili wa binadamu itatimizwa karne hii

  (GMT+08:00) 2017-02-15 19:50:09

  Katika siku zijazo vyombo vya elektroniki huenda vitawekwa ndani ya mwili wako na kurekodi data mbalimbali, msaidizi wa akili bandia anayekujua vizuri zaidi kuliko wewe atakusaidia kufanya uamuzi muhimu...

  Mwanahistoria wa Israel aliyeandika kitabu maarufu kiitwacho "historia fupi ya binadamu" Bw. Yuval Noah Harari anaona kuwa kutokana na maendeleo ya kasi teknolojia za akili bandia na viumbe, teknolojia ya kuweka mashine kwenye mwili wa binadamu itatimia karne hii, na maisha ya binadamu yatabadilika kabisa katika siku zijazo.

  Amesema mchakato huo tayari umeshaanza. Tofauti na vifaa vya jadi vikiwemo nyundo na visu, simu za mkononi aina ya Smartphone na tovuti za SNS tunazotumia ni vifaa vyenye akili, vinaweza kuelewa tabia na sifa zetu, hata kuathiri mawazo yetu. Katika miongo kadhaa ijayo, mchakato wa kuweka vifaa vya kielektroniki kwenye mwili wa binadamu utaharakishwa, na ifikapo mwaka 2100, binadamu hawataweza kuishi vizuri bila mtandao.

  Amesema kutokana na kuboreka kwa teknolojia ya kukusanya na kuchambua data, katika siku zijazo, programu za akili bandia zitachambua kila kitabu au barua pepe unayoisoma, na kurekodi mapigo ya moyo wako, hivyo zitakuelewa zaidi kuliko wewe mwenyewe, na kukusaidia kufanya chaguo zuri zaidi katika mambo makubwa ikiwemo ndoa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako