• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa Umoja wa Mataifa asema uchaguzi mkuu wa urais Somalia lazima ufanyike kwa wakati

    (GMT+08:00) 2017-01-28 19:18:52

    Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating amesema kuwa jukumu la haraka kwa sasa ni kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu wa urais nchini Somalia unafanyika kwa tarehe iliyopangwa licha ya kuwa kundi la Al-Shabaab kutoa vitisho vya kuvuruga uchaguzi huo, ikiwemo kufanya mashambulizi kadhaa ya kigaidi wiki iliyopita na kuua watu kadhaa.

    Katika taarifa yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Keating amesema mkutano wa baraza hilo uliofanyika ijumaa ulikuja kwa wakati mzuri ambao taratibu za uchaguzi wa wabunge nchini Somalia zikiendelea huku zikiwa zimebaki siku kumi na mbili kabla ya uchaguzi wa rais kufanyika.

    Pia mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa hatua za mwisho za maandalizi ya uchaguzi huo zinapaswa kufanyika kwa uwazi na kwa mujibu wa makubaliano ya sheria ili kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa wa huru na haki.

    Uchaguzi nchini Somalia umekuwa ukiahirishwa kila mara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako