• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Malaysia kuendelea kutafuta na kuokoa watalii wa China waliopata ajali ya kuzama kwa boti

    (GMT+08:00) 2017-01-30 20:02:00

    China imeitaka Malaysia kuendelea kuwatafuta na kuwaokoa watalii wa China waliopata ajali ya kuzama kwa boti ya mwendo kasi katika jimbo la Sabah nchini humo.

    China pia imeitaka Malaysia kufanya uchunguzi wa kina wa ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu watatu, na wengine kadhaa hawajulikani walipo.

    Habari zinasema wafanyakazi wawili wa boti hiyo wanashikiliwa na polisi ili kusaidia uchunguzi. Nahodha na mfanyakazi mmoja waliokolewa kwanza baada ya boti hiyo iliyokuwa na watalii 28 wa China na wafanyakazi watatu kupotea Jumamosi.

    Waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak amesema anafuatilia kwa karibu tukio hilo na kutaka uchunguzi wa kina ufanyike ili kugundua sababu yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako