• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Uingereza yatoa mpango wa kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-02-03 18:25:12

    Serikali ya Uingereza imetoa waraka ukibainisha kwa njia ya kisheria lengo la nchi hiyo kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya na pia kusisitiza umuhimu wa utulivu na taratibu za mchakato.

    Kwa mujibu wa waraka huo, Uingereza itajitoa kwenye soko la pamoja na Umoja wa Forodha barani Ulaya, lakini itatafuta uhusiano mpya wa wenzi wa kimkakati na Umoja wa Ulaya. Pia itatoa mfumo mpya wa kudhibiti wahamiaji kutoka nchi wanachama wa Umoja huo. Kwenye upande wa sheria, Uingereza itajitoa kwenye udhibiti wa mahakama ya Ulaya.

    Habari zinasema, Baraza la chini la Bunge la Uingereza Jumatano wiki hii lilipiga kura kuunga mkono mpango wa kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya uliowasilishwa na serikali na kumwidhinisha waziri mkuu wa nchi hiyo kuzindua mchakato huo mwezi Machi mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako