• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Manchester United yaichapa Leicester City Kwao

    (GMT+08:00) 2017-02-06 08:25:11

    Manchester United imewatandika Mabingwa wa England Leicester City 3-0 wakiwa nyumbani kwao King Power Stadium kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.

    Ushindi huo umewabakiza Man United Nafasi ya 6 lakini sasa wapo Pointi 1 nyuma ya Timu ya 5 Liverpool, Man United walipata Bao lao la kwanza Dakika ya 41 baada ya Kichwa cha Chris Smalling kuwahiwa na Mkhitaryan kabla Beki wa Leicester Huth kuukuta Mpira na kumtoka Beki mwingine wa Leicester Morgan na kumchambua Kipa Schmeichel.

    Sekunde 87 baada ya Bao hilo Man United walikuwa 2-0 mbele kwa Bao la Zlatan

    Hadi Mapumziko Manchester United ilikuwa ikiongoza kwa bao 2-0

    Kipindi cha Pili kuanza Timu zote zilifanya mabadiliko kwa Leicester kuwaingiza King na Gray kuwabadili Musa na Okazakina huku Man United wakimtoa Marcos Rojo na kumwingiza Daley Blind.

    Man United walifunga Bao la 3 Dakika ya 49 kufuatia ushirikiano mwema wa Ibrahimovic na Mkhitaryan kumfungulia Juan Mata kupiga Bao.

    Kwenye mechi nyingine ya EPL, Manchester City yailaza Swansea City 2-1. Gabriel Jesus alipiga Bao 2 na la pili likiwa la ushindi wakati Manchester City ikiichapa Swansea City 2-1 huko Etihad na kupanda hadi Nafasi ya 3 Ligi Kuu England.

    Jesus alifunga Bao la Kwanza Dakika ya 11 na Swansea kusawazisha Dakika ya 81 kwa Bao la Gylfi Sigurdsson.

    Huku Gemu ikielekea kuwa Sare na Bango likionyesha Dakika 4 za Nyongeza baada ya Dakika 90 kwisha, Jesus aliipa ushindi City kwa Bao la Dakika ya 92.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako