• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maharagwe yakihisi magugu yaliyopaliwa yatakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kukinga maradhi na wadudu

  (GMT+08:00) 2017-02-07 16:58:19

  Wanasayansi waliwahi kufanya utafiti kuhusu mawasiliano kati ya mimea kupitia harufu. Mimea ikiumwa na wadudu, itatoa harufu maalum, na mimea mingine iliyoko karibu ikihisi harufu hiyo, itainua uwezo wa kujilinda.

  Mwezi Julai mwaka 2012, 2013 na mwaka 2015, watafiti wa Chuo Kikuu cha Kyoto cha Japan walifanya majaribio ya kuweka magugu yaliyopaliwa kutoka sehemu nyingine karibu na mimea midogo ya maharagwe, ili kufanya mimea hiyo kuhisi harufu ya magugu hayo yaliyoharibika. Baada ya magugu hayo kukauka, watafiti waliweka magugu mapya ili kuhakikisha harufu ya magugu inakuwepo mashambani siku zote.

  Watafiti waligundua kuwa maharagwe yanayohisi harufu ya magugu yanaathiriwa na wadudu kwa mara chache zaidi kuliko maharagwe mengine, na maharagwe hayo yana kemikali nyingi zaidi ya Isoflavones. Utafiti mwingi unaonesha kuwa kemikali hiyo inasaidia binadamu kukinga saratani.

  Watafiti wamesema majaribio yao yanaonesha kwamba watu wanaweza kutumia magugu yaliyopaliwa kukinga wadudu mashambani. Utafiti huo umetolewa kwenye gazeti la ripoti za sayansi la Uingereza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako