• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Aina tatu za simu za kisasa zinazotengenezwa na China zachukua nafasi za juu katika uuzaji nchini humo

    (GMT+08:00) 2017-02-07 18:09:58

    Chapa za simu za OPPO, Huawei, na Vivo, zinazotengenezwa na China, zimeyapita makampuni ya Apple na Xiaomi na kuwa aina tatu za simu zinazouzwa zaidi nchini China kwa upande wa uuzaji kwa mwaka jana.

    Shirikisho la Takwimu la Kimataifa (IDC) limetoa ripoti ikisema, kwa mara ya kwanza, OPPO iliuza simu za mkononi milioni 78.4 nchini China mwaka jana, ikiwa ni zaidi kwa asilimia 122.2 ikilinganishwa na mwaka 2015, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na kampuni ya Huawei na Vivo ikiwa kwenye nafasi ya tatu.

    Ripoti hiyo imesema, chapa hizo zilikuwa maarufu sana kwa vijana, hususan wasichana wanaopenda kwenda na wakati, kutokana na kufanyiwa matangazo na watu maarufu.

    Kwa pamoja, chapa hizo tatu zimechukua asilimia 48 ya soko la simu za mkononi nchini China kwa mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako