• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwaka 2017 kasi ya maendeleo ya uwekezaji wa China katika nchi za nje itapungua kiasi

    (GMT+08:00) 2017-02-09 17:57:39

    Msemaji wa Wizara ya biashara ya China Bw. Sun Jiwen leo hapa Beijing amesema, uwekezaji wa moja wa moja wa China katika nchi za nje unatazamiwa kuendelea kupata maendeleo, lakini kasi yake itapungua kiasi. China inatumai kuwa nchi mbalimbali zitapinga vitendo vya kujilinda kibiashara, na kuzidi kurahisisha hatua za kuidhinisha uwekezaji kutoka nje. Wakati huo huo, China itaendelea kusukuma mbele utekelezaji wa miradi ya "Ukanda mmoja, Njia moja".

    Takwimu kutoka Wizara ya biashara ya China zimeonesha kuwa, mwaka jana thamani ya uwekezaji usio wa kifedha wa China katika nchi za nje ilikuwa dola za kimarekani bilioni 170, hili ni ongezeko la asilimia 44.1, na kasi ya ongezeko hilo ni mara tatu kuliko mwaka uliotangulia, kiasi hicho kimeweka rekodi mpya katika historia ya thamani ya jumla ya uwekezaji wa China katika nchi za nje, pia katika nchi za Marekani, Ulaya na Australia. Lakini kutokana na kushindwa kufufuka kwa uchumi wa dunia, na kurejea kwa vitendo vya kujilinda kibiashara, baadhi ya nchi zimeweka masharti makali kwa uwekezaji wa biashara kutoka nchi za nje. Msemaji wa Wizara ya biashara Bw. Sun Jiwen anasema:

    "Hivi karibuni, msukosuko katika soko la fedha la kimataifa umezidi kuwa mbaya, sera za uchumi za baadhi ya nchi haziko bayana, na baadhi ya nchi zilizoendelea zimeweka vikwazo kwa uwekezaji kutoka China hususan kwa kampuni za serikali ya China, hali ambayo imeongeza hatari kwa uwekezaji wa kampuni za China katika nchi za nje."

    Bw. Sun Jiwen pia amesema mwaka huu uwekezaji wa China katika nchi za nje utapata maendeleo katika mwaka 2017, lakini kasi yake itapungua kiasi. Wizara ya biashara ya China itaendelea kuunga mkono kampuni zenye uwezo na masharti mazuri za China kuwekeza katika nchi za nje kwa kufuata kanuni zinazohusika, kuzidi kurahisisha hatua za kuidhinisha kampuni za China kuwekeza nchi za nje, na kukinga hatari za uwekezaji huo. Pia inatumai kuwa nchi mbalimbali zitapinga aina zote za vitendo vya kujilinda kibiashara, na kuzidi kurahisisha hatua za kuidhinisha uwekezaji kutoka nchi za nje.

    Tangu mapendekezo ya ushirikiano wa "Ukanda mmoja, Njia moja" yatangazwe, miradi mbalimbali inayohusika inafuatiliwa sana. Hivi sasa ujenzi wa miradi ya kipindi cha pili cha ujenzi wa barabara nchini Pakistan, barabara kuu mjini Karachi, reli kati ya China na Laos umeanza kutekelezwa, na reli ya mwendo kasi nchini Uturuki, reli kati ya Hungary na Serbia pia inatekelezwa kwa utaratibu. Hivi karibuni, shirika la utafiti linaona kuwa kuna uwezekano kuwa Mpango wa "Ukanda mmoja, Njia moja" na miradi inayotekelezwa haitakuwa na faida. Bw. Sun Jiwen akizungumzia suala hilo anasema:

    "Ni kweli miradi hiyo imetengwa na fedha nyingi, na itachukua muda mrefu kupata faida, lakini kutokana na mtizamo wa muda mrefu, miradi hiyo ina umuhimu mkubwa katika kuongeza kiwango cha mawasiliano ya kikanda ya miundo mbinu na kuwanufaisha watu wa nchi mbalimbali walioko katika eneo hilo. Katika kipindi kijacho, tutaendelea kuhimiza kwa hatua madhubuti ujenzi wa miradi hiyo, na kukuza ushirikiano wa uwekezaji na nchi zinazohusika, ili kupata faida mapema na kuzinufaisha zaidi nchi zilizoko kwenye kanda hiyo na wananchi wao."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako