• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwezi Januari thamani ya uagizaji wa bidhaa wa China kutoka nje na uuzaji wa bidhaa kwa nje zilizidi kuliko ilivyotarajiwa

    (GMT+08:00) 2017-02-10 18:00:48

    Takwimu zilizotolewa leo na Idara kuu ya Forodha ya China zimeonesha kuwa, mwezi Januari mwaka 2017, thamani ya jumla ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje na uuzaji wa bidhaa kwa nje ilikuwa RMB yuan trilioni 2.2, hili ni ongezeko la asilimia 19.6 kuliko mwaka jana wakati kama huu. Ikihesabiwa kwa dola za kimarekani, katika mwezi Januari thamani ya uuzaji wa bidhaa wa China katika nchi za nje iliongezeka kwa asilimia 7.9, hii imeonesha kuwa, hali ya kushuka kwa thamani hiyo kwa miaka 8 mfululizo imekomeshwa. Wachambuzi wanaona kuwa hali hii inakadiria kuwa thamani ya jumla ya biashara nje ya China kwa mwaka huu itakuwa nzuri zaidi kuliko mwaka jana, lakini bado inapaswa kuzingatia changamoto mbalimbali.

    Takwimu hizo zimeonesha kuwa, katika mwezi Januari, ikihesabiwa kwa sarafu ya China RMB, thamani ya jumla ya bidhaa zinazoagizwa ndani ya nchi na zinazouzwa nje ilikuwa RMB trilioni 2.2, hili ni ongezeko la asilimia 19.6 kuliko mwaka jana wakati kama huu. Ikihesabiwa kwa dola za kimarekani, thamani ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi iliongezeka kwa asilimia 7.9 kuliko mwaka jana wakati kama huu, na inakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 3.2.

    Naibu mkurugenzi wa Idara ya utafiti kuhusu soko la kimataifa katika Taasisi ya Wizara ya biashara ya China Bw. Bai Ming anaona ongezeko hilo linatokana na kufufuka kwa soko la kimataifa na kuongezeka kwa mahitaji katika soko. Anasema:

    "Kupanda kwa bei ya bidhaa katika soko la kimataifa kunachangia ongezeko la thamani ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, tena kutokana na sera mfululizo za China zinazolenga kutuliza ongezeko la uchumi, mahitaji ya China katika soko la kimataifa pia yameongezeka, hali ambayo pia inahimiza ongezeko hilo."

    Naibu mchumi mkuu wa Kituo cha kimataifa cha mawasiliano ya kiuchumi cha China Bw. Xu Hongcai anaona kuwa, hali ya biashara nje ya China kwa mwaka 2017 itakuwa nzuri zaidi kuliko mwaka 2016. Anasema:

    "Kutokana na marekebisho ya kimuundo, na kiwango cha juu zaidi cha uwazi cha maeneo ya biashara huria, thamani ya bidhaa zinazouzwa katika nje ya nchi imaonezeka."

    Takwimu kutoka Idara ya Forodha zinaonesha kuwa, katika robo ya pili ya mwaka 2017, shinikizo linaloukabili uuzaji wa bidhaa wa China katika nchi za nje linatazamiwa kupungua kiasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako