• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Roketi ya Falcon 9 yapangwa kurushwa kutoka jukwaa lililowahi kurushia roketi ya kwanza iliyopeleka binadamu mwezini

    (GMT+08:00) 2017-02-13 16:46:41

    Kampuni ya SpaceX ya Marekani imetangaza kuwa roketi ya Falcon 9 imewekwa kwenye jukwaa la kurushia roketi la 39A katika kituo cha safari ya anga ya juu ya Kennedy. Roketi hiyo itarushwa angani tarehe 18 kwa mujibu wa mpango, na itapeleka chombo cha mizigo cha Dragon kwenda kituo cha safari ya anga ya juu ya kimataifa.

    Mkurungenzi mtendaji mkuu wa kampuni ya SpaceX Bw. Elon Musk aliweka picha ya roketi ya Falcon 9 kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema, roketi ya Saturn V iliyopeleka binadamu mwezini kwa mara ya kwanza mwaka 1969 ilirushwa kutoka jukwaa la kurushia roketi la 39A, na kampuni yake inaona fahari kubwa kuruhusiwa kutumia jukwaa hilo.

    Katika miaka mingi iliyopita, vyombo vingi vya safari ya anga ya juu aina ya space shuttles vya NASA vilirushwa kutoka jukwaa hili. Mwezi Julai mwaka 2011, NASA ilirusha chombo cha safari ya anga ya juu cha Atlantis kutekeleza jukumu la mwisho la mradi wa space shuttles. Baada ya mradi huo kumalizika, jukwaa hilo halikutumiwa tena. Mwaka 2014, kampuni ya SpaceX ilisaini mkataba na NASA kukodi jukwaa hili kwa miaka 20. Baada ya kufanyiwa utengenezaji na uboreshaji, sasa jukwaa hili liko tayari kutumiwa tena.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako