• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga kithabiti ziara ya wabunge wa Taiwan nchini India

    (GMT+08:00) 2017-02-15 19:51:57

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema China imetoa malalamiko makali kwa India, kufuatia ziara ya wabunge wa Taiwan nchini India, na kutarajia India kuheshimu na kuelewa mambo muhimu yanayofuatiliwa na China, na kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja.

    Habari zinasema wabunge watatu wa Taiwan wako ziarani nchini India, na baadhi yao wametaja suala la kuinua hadhi ya idara za Taiwan nchini India. Bw. Geng Shuang amesisitiza kuwa China inapinga kithabiti nchi zenye uhusiano wa kibalozi na China kufanya mawasiliano ya kiserikali na Taiwan..

    Jana pia wizara ya elimu, utamaduni, michezo, sayansi na teknolojia ya Japan ilitoa mwongozo wa mafundisho kwa shule za msingi na sekondari ikisema kisiwa cha Diaoyu ni ardhi ya Japan. Bw. Geng Shuang amesisitiza kuwa kisiwa cha Diaoyu na visiwa vinavyokizunguka ni ardhi ya China, na kuitaka Japan iheshimu historia, na kuacha vitendo vya uchokozi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako